Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Mti wa Tumbaku Nicotiana glauca – mmea wa roshani wenye tumaini!

foto

Tumbaku (Nicotiana glauca)

Hitaji la mwanadamu kufanya kitu kipya na kisicho cha kawaida halizuiliki. Hivyo wakulima wa bustani pia wanaota kulima kitu kipya kwenye bustani zao – kitu ambacho hakuna mtu mwingine mwenye nacho. Soko la mimea kwahiyo huwapa wakulima wa bustani kitu kipya kila siku – kuiba njaa ya wakulima wa bustani kutafuta kitu Fulani cha asili kutosheleza mahitaji yao. Uzinduzi wa kibiashara wa aina mpya utaufanya mmea wa tumbaku kujulikana kwa wakulima wote wa bustani hivi karibuni.

Ijumaa 8.7.2011 15:38 | chapa | Mimea ya kigeni

Kiwano – Cucumis metuliferus

Kiwano ni tunda lenye urefu wa sentimeta 10–15 linalofanana na machungwa. Iko kwenye familia ya tango. Tunda lina miba midogo midogo kwenye ganda kumfanya mtu afikirie silaha za zama za kati. Nyama ya tunda ni ya kijani na kwa kawaida ina mbegu nyingi nyeupe zenye urefu wa sentimita. Likiwa halijaiva bado, rangi ya tunda ni kijani.

Jumatano 6.7.2011 15:34 | chapa | Mimea ya kigeni

Chai ya China – Lima chai yako mwenyewe!

foto

Chai ya China

Kabla ya kipindi cha baridi kumalizika, kila mkulima wa bustani anazingatia kipi ataota katika msimu ujao. Unaona hakuna changamoto tena kulima nyanya, pilipili mboga na tango? Unataka kitu kingine? Kitu kingine kisicho cha kawaida? Unafikiriaje wazo la kulima chai yako mwenyewe?!

Jumanne 5.7.2011 15:00 | chapa | Konifa

Embe Kalimantan, Kasturi (Mangifera casturi)

Embe Kalimantan (Mangifera casturi) au kienyeji unajulikana kama Kasturi ni tunda la mti wa matunda ya msimu wa joto, wenye urefu wa takribani mita 10–30, unapatikana kwenye eneo dogo la Banjarmasin, Kusini mwa Borneo (Indonesia). Siku hizi miti hii imeadimika sehemu za porini kutokana na kukatwa katwa kinyume cha sheria. Hata hivyo bado inalimwa kwa kiasi kidogo katika eneo hili kutokana na utamu wa matunda yake.

Jumatatu 7.9.2009 12:48 | chapa | Mimea ya kigeni

Kukuza mwembe kutoka mbegu

Unatakiwa kupanda mbegu iliyovunwa vizuri, ili kupata matokeo mazuri ya uotaji. Loanisha mbegu kwenye maji yenye kiwango cha joto karibu nyuzijoto 20–25 kwa muda wa takribani saa 2–6.

Jumanne 1.9.2009 07:01 | chapa | Mimea ya kigeni

Maembe ya Indonesia

Katika Kisiwa cha Borneo huko Indonesia kuna spishi za mwembe zipatazo 34 (Mangifera) ambazo hutokea kiasili kwenye kisiwa. Idadi kubwa ya spishi hizi ziko hatarini kupotea kutokana na uharibifu wa misitu. Baadhi ya spishi kama vile Kalimantan Mango (Mangifera casturi) tayari imepotea porini.

Jumatatu 31.8.2009 17:30 | chapa | Mimea ya kigeni

Indian Lotus (Nelumbo nucifera)

foto

ua ya Indian Lotus

Indian Lotus (Nelumbo nucifera) ni mmea unaovutia wa majini wenye majani ya rangi ya kijani yanayoelea juu ya maji. Maua ya rangi ya waridi kwa kawaida yanapatikana kwenye mashina myembamba yanayokua kwa sentimeta kadhaa juu ya maji.

Maua ya Indian Lotus hutumika na wafuasi wa madhehebu ya Budha wakati wa sherehe za kidini. Mmea wote hufaa kwa matumizi ya binadamu, ingawa hasa mbegu na mzizi hutumika kwenye mapishi ya kitamaduni Kusini-Mashariki yote ya Asia. Indian Lotus ni mmea wa paludal ambapo unaweza kuoteshwa kama vile unavyooteshwa lily ya majini yanayonukia. Siyo vigumu kuotesha mmea huu kwenye hali zetu; mtu ni lazima ajue ni kwa namna gani!

Jumapili 9.8.2009 11:54 | chapa | Mimea inayotumia maji mengi na mimea ya majini

Michikichi inayostahimili baridi Rhapidophyllum hystrix

Rhapidophyllum hystrix ni spishi kuu ya mchikichi inayostahimili baridi kali. Kuna spishi moja tu kwenye jenasi Rhapidophyllum. Maskani ya asili ya mchikichi huu ni maeneo yenye unyevunyevu ya sehemu za Kusini- Mashariki mwa Marekani. Hata hivyo, shukrani kwa tabia yake ya kuvumilia baridi kali ambayo iko chini kama nyuzi joto – 20, ni mmea wa bustani unaojulikana sana duniani, hasa hasa Ulaya.

Jumapili 9.8.2009 11:39 | chapa | Michikichi

Michikichi Parajubaea torallyi

Parajubaea torallyi ni mchikichi mgumu wa kuvutia kutoka Marekani ya Kusini. Hata hivyo, hulimwa kwa kiwango kidogo nje ya eneo lake la asili, Bolivia, kutokana na ukubwa wa mbegu zake ambazo usafirishaji wake unatumia gharama kubwa.

Jumapili 9.8.2009 11:36 | chapa | Michikichi

Khasi Pine (Pinus kesiya)

Khasi Pine (Pinus kesiya) ni spishi inayokua haraka sana kutoka Asia, ambayo mara nyingi haipatikani kwenye maeneo mengine nje ya nchi yake. Miti hii ina urefu wa takribani mita 30–35 na magogo yake yanaweza kufika hadi upana wa m 1. Kila tawi lina spines tatu – kila mmoja una urefu wa karibu sm 15 hadi 20. Matunda ya miti hii ina urefu wa karibu sm 5 hadi 9 na mbegu zake karibu sm 1,5 hadi 2,5.

Jumapili 9.8.2009 11:23 | chapa | Konifa

Kurasa: 1-10 11-20 21-22

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.