Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Hifadhi ya makala zote

Hapa utaona makala zote zinazopatikana kwenye Botanix zikiwa zimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

Category: zote Konifa Maelekezo juu ya uoto wa mimea Majani Michikichi Mimea inayotumia maji mengi na mimea ya majini Mimea ya kigeni Uyoga Wadudu

Author:

2011

Julai (13)

Kundi: Mimea ya kigeni

Mimea ya kigeni

Welwitschia mirabilis – ukulima wa kisukuku

foto

Welwitschia

Welwitschia (Welwitschia mirabilis) ni mmea wa kale unaolimwa katika eneo dogo la ukanda wa mkoa wa pwani wa Bahari ya Atlantic nchini Namibia na Kusini mwa Angola. Welwitschia kiukweli ni mti, ingawa hauonekani kama mti kwa mtazamo wa haraka wa kwanza. Mmea wote una shina moja fupi ambalo hutoa majani mawili – haya yanaonekana kama riboni mbili kubwa zenye mawimbi yaliyochakaa, ncha kumba. Welwitschia wakati mwingine unaonekana kama rundo takataka!

Jumanne 26.7.2011 10:32 | chapa | Mimea ya kigeni

Cherimoya (Annona cherimola)

Ni aina ya matunda ya joto yanayovutia yanayoingizwa Ulaya sasa. Nimefanikiwa kununua tunda la cherimoya na kulionja. Halipatikani kwenye mduka ya matunda lakini shukrani kwa ladha yangu mwenyewe nzuri, litapata sehemu yake pale vile vile!

Jumatano 20.7.2011 16:48 | chapa | Mimea ya kigeni

Mti wa Tumbaku Nicotiana glauca – mmea wa roshani wenye tumaini!

foto

Tumbaku (Nicotiana glauca)

Hitaji la mwanadamu kufanya kitu kipya na kisicho cha kawaida halizuiliki. Hivyo wakulima wa bustani pia wanaota kulima kitu kipya kwenye bustani zao – kitu ambacho hakuna mtu mwingine mwenye nacho. Soko la mimea kwahiyo huwapa wakulima wa bustani kitu kipya kila siku – kuiba njaa ya wakulima wa bustani kutafuta kitu Fulani cha asili kutosheleza mahitaji yao. Uzinduzi wa kibiashara wa aina mpya utaufanya mmea wa tumbaku kujulikana kwa wakulima wote wa bustani hivi karibuni.

Ijumaa 8.7.2011 15:38 | chapa | Mimea ya kigeni

Kiwano – Cucumis metuliferus

Kiwano ni tunda lenye urefu wa sentimeta 10–15 linalofanana na machungwa. Iko kwenye familia ya tango. Tunda lina miba midogo midogo kwenye ganda kumfanya mtu afikirie silaha za zama za kati. Nyama ya tunda ni ya kijani na kwa kawaida ina mbegu nyingi nyeupe zenye urefu wa sentimita. Likiwa halijaiva bado, rangi ya tunda ni kijani.

Jumatano 6.7.2011 15:34 | chapa | Mimea ya kigeni

Embe Kalimantan, Kasturi (Mangifera casturi)

Embe Kalimantan (Mangifera casturi) au kienyeji unajulikana kama Kasturi ni tunda la mti wa matunda ya msimu wa joto, wenye urefu wa takribani mita 10–30, unapatikana kwenye eneo dogo la Banjarmasin, Kusini mwa Borneo (Indonesia). Siku hizi miti hii imeadimika sehemu za porini kutokana na kukatwa katwa kinyume cha sheria. Hata hivyo bado inalimwa kwa kiasi kidogo katika eneo hili kutokana na utamu wa matunda yake.

Jumatatu 7.9.2009 12:48 | chapa | Mimea ya kigeni

Kukuza mwembe kutoka mbegu

Unatakiwa kupanda mbegu iliyovunwa vizuri, ili kupata matokeo mazuri ya uotaji. Loanisha mbegu kwenye maji yenye kiwango cha joto karibu nyuzijoto 20–25 kwa muda wa takribani saa 2–6.

Jumanne 1.9.2009 07:01 | chapa | Mimea ya kigeni

Maembe ya Indonesia

Katika Kisiwa cha Borneo huko Indonesia kuna spishi za mwembe zipatazo 34 (Mangifera) ambazo hutokea kiasili kwenye kisiwa. Idadi kubwa ya spishi hizi ziko hatarini kupotea kutokana na uharibifu wa misitu. Baadhi ya spishi kama vile Kalimantan Mango (Mangifera casturi) tayari imepotea porini.

Jumatatu 31.8.2009 17:30 | chapa | Mimea ya kigeni

Mti wa mfune wa India Pongamia pinnata

foto

Pongamia pinnata

Mti wa mfune wa India Pongamia pinnata (majina mengine ya kienyeji: mti wa Honge, mtu wa Pongam, Panigrahi) una urefu wa takribani mita 15 –25, inapatikana kwenye familia ya Fabaceae. Ni mkubwa sehemu ya juu na maua madogo madogo mengi ya rangi nyeupe, waridi au urujuani. Asili yake ni India, lakini inaoteshwa kwa kiwango kikubwa Kusini – Mashariki mwa Asia.

Jumamosi 8.8.2009 09:27 | chapa | Mimea ya kigeni

Shelisheli Artocarpus odoratissimus, Marang

Jenasi Shelisheli (Artocarpus) ina takribani spishi 60 za miti ya kitropika isiyokauka kutoka kwenye familia ya Moraceae (familia ya forosadi au familia ya mtini). Inatokea Kusini Mashariki mwa Asia na kwenye visiwa vya bahari ya Pasifiki. Shelisheli inahusiana kwa karibu na Ficus (mtini). Shelisheli inayolimwa sana ni Artocarpus altilis. Nyingine baadhi kama vile Artocarpus communis, Artocarpus integer (Cempedak), Artocarpus heterophyllus (Jackfruit, Nangka) na Artocarpus odoratissimus (Marang) pia ni sehemu ya familia ya shelisheli.

Ijumaa 7.8.2009 11:16 | chapa | Mimea ya kigeni

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.