Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Shelisheli Artocarpus odoratissimus, Marang

Jenasi Shelisheli (Artocarpus) ina takribani spishi 60 za miti ya kitropika isiyokauka kutoka kwenye familia ya Moraceae (familia ya forosadi au familia ya mtini). Inatokea Kusini Mashariki mwa Asia na kwenye visiwa vya bahari ya Pasifiki. Shelisheli inahusiana kwa karibu na Ficus (mtini). Shelisheli inayolimwa sana ni Artocarpus altilis. Nyingine baadhi kama vile Artocarpus communis, Artocarpus integer (Cempedak), Artocarpus heterophyllus (Jackfruit, Nangka) na Artocarpus odoratissimus (Marang) pia ni sehemu ya familia ya shelisheli.

Katika makala hii tutatambulisha kwako Marang (Artocarpus odoratissimus). Ni mti usiokauka kutoka kisiwa cha Borneo huko Indoneshia. Hata hivyo, imekuwa ikizalishwa kwa kiwango kikubwa kwa ajili ya masoko ya ndani katika nchi za Malesia, Tailandi na Ufilipino. Kwa lugha za asili inajulikana kama Atau, Keiran, Loloi, Madang, Marang, Pi-ien, Pingan, Tarap, Terap, na Khanun Sampalor. Spishi hii haifahamiki nje ya nchi hizo zilizotajwa. Sehemu za porini miti hii huota kwenye udogo wenye mchanga, kwenye misitu iliyopo umbali wa m 1000 kutoka kwenye usawa wa bahari.

Kwa kawaida miti ya Artocarpus odoratissimus hukua hadi kufikia urefu wa mita 25; majani yake huwa na urefu wa sm16 hadi 50 na upana wa sm11 hadi 28.

Mche mmoja unatosha katika kuzalisha matunda. Matunda ya mti huu ni ya kijani, umbo la mviringo, urefu wa sm 16 na upana sm13, uzito wake kwa kila tunda ni karibu kg 1. Tunda hili linaweza kuliwa likiwa bichi au baada ya kupikwa, lakini mbegu zake ni lazima zipikwe kabla ya kuliwa.

Shelisheli ni aina kuu ya chakula kwa watu wa Kusini Mashariki mwa Asia. Ndani ya tunda kuna rangi nyeupe kama theluji, na tunda lenyewe ni tamu sana na lina harufu nzuri, linanukia kama Durian (Durio, ni tunda kuu linalonukia vizuri duniani)

Njia nzuri ya kuotesha Marang Artocarpus odoratissimus ni kwa kutumia mbegu. Mbegu mpya zinaota vizuri na kuchipua ndani ya wiki. Hata hivyo, kuna uwezekano wa mbegu kuwa mbaya baada ya kuhifadhiwa kwa takribani wiki tatu. Kwa hiyo, mbegu lazima zipandwe kwenye mchanga mchanga, udondo uliokauka vizuri mara tu baada ya kuvunwa. Uenezaji uoto hufanikiwa kwa kiwango kidogo kutokana na miti hii kushambiliwa na wadudu na magonjwa.

Shelisheli haistahimili hali ya baridi. Kutokana na uasili wake wa kitropiki, kiwango cha chini cha joto kisishuke chini ya nyuzi joto 7. katika maeneo yenye hali ya kitropiki au joto kidogo, Mshelisheli unaweza kupandwa kwenye bustani, lakini kama sehemu husika ina baridi kali basi ni lazima uwekwe ndani au kwenye nyumba ya kuhifadhi mimea.


Makala inayofuata: Mti wa mfune wa India Pongamia pinnata »»»

Ijumaa 7.8.2009 11:16 | chapa | Mimea ya kigeni

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.