Cherimoya (Annona cherimola)
Ni aina ya matunda ya joto yanayovutia yanayoingizwa Ulaya sasa. Nimefanikiwa kununua tunda la cherimoya na kulionja. Halipatikani kwenye mduka ya matunda lakini shukrani kwa ladha yangu mwenyewe nzuri, litapata sehemu yake pale vile vile!
Cherimoya ni majina ambayo kwa kawaida hutumika sana kwa matunda ya Annona cherimola ambayo hulimwa kwenye mabonde ya Andes kutoka Colombia hadi Peru kwenye mwinuko wa m 700–2400 kutoka usawa wa bahari. Pia huishi kwenye hali ya chini ya joto na kwa hiyo inaweza kulimwa kwa kiwango kikubwa kwenye maeneo mingine ya joto duniani – hata Israel na Kusini mwa Hispania. Ndani ya aina hii tunajua karibu aina 120.
Cherimoya ina gamba la kijani kahawia na juu yake sio kawaida kama vile mtu ameacha alama zake za vidole. Matunda ya kijani yanaweza kuhifadhiwa kwenye chumba cha hali ya joto. Nyama ya tunda ni ya sasa hivi, ina rangi ya maziwa na ina ladha kama ndizi na/au nanasi. Ndani ya tunda kuna mbegu nyekundu 10–20 kubwa kama maharage. Tunda huliwa hasa likiwa bichi.
Unaweza kupanda mbegu nyumbani kwako au nyumba ya kuhifadhia mimea. Uotaji wake unatofautiana, lakini kwa kawaida unadumu kati wiki au wiki tatu. Hali ya hewa nzuri kwa ajili ya uotaji ni nyuzijoto 27. Mimea michanga ina rangi ya nyekundu, lakini hubadilika haraka kuwa rangi ya kijani iliyofifia na majani yenye umbo la yai iliyofunikwa na nywele ambayo yana urefu wa sm 10–15 na majani marefu nyuma yake.
Wakati wa baridi mmea hupoteza majani yake na yanapoharibika hunukia isivyokawaida kidogo. Matawi mapya huota mahali ambapo majani yameanguka. Aina zote za annona hudai mwanga mwingi na njia maalumu ya kufichwa – hii ni kama hatua ya majadiliano baina ya wakulima! Binafsi naweka annona kwenye sehemu yenye kiwango cha joto cha nyuzijoto 10–15 kuficha. Wakati wa baridi mtu anatakiwa kuangalia hatua ya ukuaji wa mimea tofauti mfano kwenye joto la chumba, kuangalia ipi itachanua ya kwanza.
Annona huchanua mara tatu hadi tano kwa mwaka. Kabla ya kuchanua, annona huonekana kusinyaa na kupoteza karibu majani yake yote. Maua yake ni rangi ya njano kahawia na huchanua majani yanapoanguka au huchanua pamoja na majani mapya. Kwa mchavusho mimea miwili inahitajika na uivaji wa matunda huchukua kati ya miezi 5–7.
Usisumbuliwe na eneo la juu la mmea ambalo wakati wote huonekana kusinyaa. Kipindi kifupi cha ukame hakitakuwa kibaya kwa mmea, lakini unahitaji maji wakati wa baridi vile vile. Kama una bahati, unaweza pia kununua moja ya aina zifuatazo:
Annona squamosa – annona yenye ganda ambalo lina tunda lenye ganda kama nanasi. Haya pia yanaitwa sugar apples na tunda lina rangi ya njano kijani.
Annona muricata – annona hii ina matunda ya joto yanayokua kwenye gome la mmea na ni makubwa (kg 1,5–5) – ina miba yenye urefu wa sm 0,5 iliyojikunja. la kijani. Chai ya inayojulikana kwa jina la Corosol tea hutengenezwa kutokana na majani ya mmea huu.
««« Makala iliyopita: NOVODOR FC kwa kupambana na mdudu aina ya Colorado anayeharibu nyanya Makala inayofuata: Ulimaji wa Klova ya majani manne - (Marsilea quadrifolia) »»»
Jumatano 20.7.2011 16:48 | chapa | Mimea ya kigeni
Kuhusu KPR
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.