Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Ulimaji wa Klova ya majani manne - (Marsilea quadrifolia)

foto

Marsilea quadrifolia

Klova ya majani Manne (Marsilea quadrifolia) ni jani la maji ambalo majani yake yanaonekana kama klova. Unadhani kwamba maneno jani la maji na klova hayahusiani? Hasha – maneno yote yanaelezea tabia za mmea huu usiyo wa kawaida na upambao ulimwengu wa bustani.

klova ya majani manne una rizomu ndefu, ambayo hufanya mtu afikirie gidamu. Majani ambayo yanaelea juu ya maji, yanaua kutoka kwenye rizomu. Majani haya yamegawanyika katika sehemu nne, kufanana na klova ya majani manne. Unapotoa rizomu nje ya maji katika msimu wa kupukutisha majani, vitu vichache vidogo huonekana (vinafanana namaharage madogo). Ni matunda ambayo yana vijimbegu – kuanzia pale mwisho kwamba mimea hii huweka tawi kutoka kwenye majani. Klova ya majani mannekwenye maji yaliyosimama, yana virutubisho vingi, kwenye mabara yote, isipokuwa Marekani ya Kusini.

Marekani, mmea huu unachukuliwa kama mmea mwingiliaji. Slovakia mmea huu hulimwa kwenye maeneo 7 kwenye ufuko wa mto Latorica. Hapo zamani, umeonekana kwenye eneo la mto Bodrog, Laborec na Uh.

Kwenye maeneo ya joto kuna aina inayohusiana na hiyo, hii wakati meingine huoteshwa kwenye tanki la maji la kuwekea mimea..

Klovu ya majani manne (Marsilea quadrifolia), kuhusu ulimaji, syo mmea unaodai sana na hutosheka zaidi na chungu chochote ili mradi kijazwe maji na udongo kidogo chini. Unaweza kuoteshammea huu bila tatizo lolote kwenye chungu cha sm 20×20×20, lakini saizi nzuri ya chungu ni cha lita 60–80 au zaidi. Unawezapiakuweka mmea huu nje katika kipindi chote cha mwaka (kwani inavumilia barafu). Kwakuwa siyo mmea unaodai, na hukua kwa urahisi, kila mtu anaweza kuotesha. .

foto

Klova ya majani manne utakua vizuri kwenye dimbwi la bustani. Weka tu udongo kidogo kutoka kwenye bustani yako chini ya dimbwi – kisha weka rizomu kwenye udongo. Baada ya hapo, uangalizi mdogo sana unahitajika, kwani klovayamajani manne utajiangalia wenyewe. Klova ya majani manne utazoea kwa urahisi kwenye kiwango cha maji na ubora wa maji haujaliwi sana na mmea. Unaweza kuotesha kwenye vina mbalimbali (sm 5–100) – matawi ya mmea yatazoea kina cha maji hadi majani yake yatakapoelea juu ya maji. Unaweza kuusaidia mmea kuenea kwa kupasua rizomu. Rizomu kidogo (karibu sm 10) inatosha kutengeneza zulia la klova la majani manne juu ya maji.

««« Makala iliyopita: Cherimoya (Annona cherimola) Makala inayofuata: Upandaji wa nyasi kwenye uwanja mpya »»»

Alhamis 21.7.2011 14:50 | chapa | Mimea inayotumia maji mengi na mimea ya majini

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.