Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Ufanye nini na majani yaliyofyekwa?

Kama unapenda zulia zuri lenye majani ya chini, hakika utafyeka nyasi za uwanja wako kila mara. Kwa sasa, ufyekaji majani wa mara kwa mara unazalisha kiwango kikubwa cha majani ambayo yanakusumbua tu. Wakulima wengi wa bustani ninaowafahamu wanaondoa majani yao na takataka za nyumba zao. Naweza kutikisa Kichwa changu tu katika kutoamini watu ambao pasipouangalifu wanatupa mbolea rahisi!

Majani ni mazuri kwa vitu vingi, ambapo mbolea ni moja vitu vya thamani sana (hii inajumuisha majani, samadi, magome yaliyokauka kutoka kwenye mashina ya miti n.k.) na inatumika kufunika mimea maalumu na maua. Mbolea hii huzuia kuvukizwa kwa maji mengi, hutunza unyevunyevu kwenye udongo kwa muda mrefu na kutengeneza hali nzuri kwa vijiumbe vyenye manufaa. Majani yaliyofyekwa ambayo tunafunikia mimea, hupeleka virutubisho, ambavyo vinachukuliwa na mimea kwa urahisi.

Mbolea hii inaweza kuzuia kupasuka kwa matunda ya nyanya na uasili wake kitaalamu sana. Unapotumia majani kama smadi unaweza kuzuia matunda yale madogo na zabibu kuanguka mapema wakati wa kipindi cha ukame – kama mwaka huu kwa mfano. Magome ya msonobari yaliyokauka hayana viini vya virutubisho na hivyo hutumika tu kufunikia mbuga,bustani n.k.

««« Makala iliyopita: Jinsi gani ya kufyeka nyasi za uwanja wako kwa usahihi? Makala inayofuata: Upandaji wa matunguu na miche ya maua »»»

Ijumaa 22.7.2011 08:54 | chapa | Majani

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.