Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Upandaji wa matunguu na miche ya maua

Toa matunguu ya maua na miche ambayo umepokea kwa njia ya postaat kutoka kwenye vifurushi, na iache ikiwa imesimama kwenye kivuli kwa takribani siku 2–3. Uwezekano wa pili ni kuipanda haraka na kuiweka kwenye kivuli kwa siku chache ili isipatwe na mwanga wa jua moja kwa moja.

Kupanda miche

Tengeneza mfuo mdogo kupanda miche ndani yake. Itoe miche nje ya chungu (hivyo kutoka kwenye mfuko wa plastiki iwapo miche imepakiwa tofauti), geuza mizizi iangalie chini na isambaze kabla ya kuweka mmea wote kwenye mfuo.

Mimina maji kwenye mfuo na baada ya udongo kunyonya maji yote, mimina maji zaidi. Hudumia mimea mingine yote sawasawa. Baada ya kumaliza mimea yote, imwagilie maji tena.

Siku chache za mwanzo baada ya kupanda, unaweza tu kuimwaimwagilia kutokana na uhitaji na kuiangalie vizuri ukihakikisha kwamba imekingwa dhidi ya mwanga mkali wa jua. Mimea itakuatengeneza mizizi ndani ya wiki 1–3 na baada ya hapo unaweza kuiangalia kwa namna sawa kwamba unaihudumia mimea migine yote kwenye bustani.

Kupanda matunguu na miche ya maua

Kwanza chimba udongo sehemu unayotaka kupanda matunguu na mizizi (tutatumia neon la tunguu katika maelezo yafuatayo). Toa matunguu kwenye mifuko ya karatasi kabla ya kutaka kupanda. Chimba shimo la kutosha (angalia jedwali) na weka tunguu kwenye shimo huku sehemu ya juu ikiangalia juu. Baadhi ya matungu haitadumu iwapo unaipanda huku sehemu ya juu ikiwa inaangalia chini – kuwa makini kuipanda kwa usahihi!

Kama unapanda tulips katikati ya masimu wa joto (labda huwezo kuhifadhi kokte au unaenda likizo) huhitaji kuipa maji. Matunguu itapumzika na itaanza kukua tu baada ya mvua ya msimu wa kwanza wa kupukutika majani kunyesha.

Matunguu madogo ambayo ni magumu zaidi kukua, inatakiwa kupandwa ndani kidogo. Kutambua ni urefu wa kiasi gani unahitajii kupanda, ni muhimu kutambua umbali kati ya sehemu ya juu ya tunguu na sehemu ya juu ya ardhi!

Tunaoa matunguu kutoka kwenye udongo wakati sehemu ya juu (juu ya uso wa dunia) imenyauka (hii ni Sheria kwa matunguu ya maua yote isipokuwa Gladiolus) – hii inaweza kuwa jambo rahisi mapema kama Mei huko Ulaya (katika hali ya joto na ukame). Aina nyingi zinaweza kuhifadhiwa baada ya kutolewa kwenye udongo. (ilimradi ziwekwe zikiwa kavu) hadi majira ya kupukutika kwa mahani (hasa vitunguu, vitunguu swaumu, zafarani na tulips).

Aina zilizosalia kama vile yungiyungi, zabibu (Muscari), Ornithogalum, na solomon's seal (Polygonatum) zinaweza hata hivyo zisihifadhiwe kwa namna hii, kwani hazitadumu. Aina ambayo haiwezi kuhifadhiwa (kwenye sehemu kavu) ingeweza kupandwa kutoka sehemu moja kwenye bustani yako kwenda sehmu nyingine (zitadumu kwa takribani wiki moja, lakini haishauriwi kuziweka nje kwa muda mrefu zaidi ya huu).

Aina kipindi cha kupanda urefu wa mmea kwenda chini katika sm
Aina ndogo yenye tunguu la kipimo cha sm 2 kama Allium carinatum, flavum, molly, oleraceum, scorodoprasum 7.-10. 5–8
Aina kubwa yenye tunguu la kipimo cha sm 10 kama Allium giganteum, karataviense, nigrum 7.-10. 10–15
Colchicum – aina ambayo huchanua wakati wa msimu wa kupukutisha majani 8. 15
Crocus – aina ambayo huchanua wakati wa majira ya kuchipua (Crocus chrysanthus, Crocus vernus) 10. 9
Crocus – aina ambayo huchipua wakati wa msimu wa kupukutisha majani (Crocus sativius) (7.-)8. 9
Gladiolus (garden hybrids) 4.-5. 10 (ndogo zaidi ya 5)
Gladiolus (aina ya porini ya asili yake Afrika ya Kusini) 9. 5–8
Lilium candidum – yungiyungi nyeupe au Madonna lily 8. 3
Lilium – garden hybrids 9.(-10.) 5–15 kutegemea na aina
Muscari – zabibu 7.-10. 8–10
Narcissus – nasisi 8. 10
Ornithogalum umbellatum – Nyota-ya-Bethlehem, Grass Lily 7.-10. 10
Polygonatum – salomons seal 8.10., 2.-3. 10
Tulips yenye matunguu madogo kama Tulipa chrysantha, tarda, saxatillis, turkestanica, urumiensis 10. 10
Tulip yenye matunguu makubwa – Tulipa greigii, Tulipa fosteriana, Tulipa kaufmanniana na garden hybrids 10. 12–14

Lily propagation by scales

foto

Propagation of the lily by scales

Namna rahisi sana katika kuzidisha yungiyungi kwa njia ya kutumia magamba (matabaka ya tunguu)

Panda magamba kwenye mikondo ya sm1–2 kwenda ndani (= urefu wa udongo kufunika magamba) na yaweke kwenye kiwango cha joto nyuzijoto 25–30 kwa mchana na usiku nyuzijoto 22 (hali ya joto ys usiku inaweza kuwa chini, cha muhimu sana ni hali ya joto la mchana) kwenye kabati mfano, nyumba ya kuhifadhia mimea au kizingiti cha dirisha ndani ya nyumba yako. Uwache udongo ukiwa mkavu. Kwa njia matunguu mapya yatakua kwa haraka chini ya magamba. Katika mwezi 1–3, matunguu 2–3 ya sm1 yanaweza kutokea kwenye moja ya mgamba haya! Kama magamba utakuwa umeyachuna na kuyapanda mwisho wa mwezi Julai, unaweza kuyatoa matunguu haya mapyakwenye ardhi mwezi Septemba na kuyapanda shimo la sm2 bustanini. Panda kila tunguu jipya peke yake, na acha takribani sm 4 kati ya tunguu na tunguu – baada ya miaka 4–6 utakuwa na matungu maua mazuri sana yakiwa yamechanua!

Upandaji wa mbegu za matunguu ya maua

Baadhi ya matunguu ya maua yanaweza kuzalishwa kwa haraka sana na kwa usahihi kwa kutumia mbegu. Nchini Ulaya muda sahihi wa kupanda mbegu karibu sm 0,5–1 kwa ndani ni wakati wa Machi na Aprili. Usizipande katika mwaka wa kwanza, bali ziache zinapokuwa kwenye maene yake ya asili. Baadhi ya aina zitakuwa zimechanua tayari msimu ujaop. Aina nyingi hata hivyo zitaanza kuchanua miaka 2–5 baada ya kupandwa. Aina ndogo itachanua mapema zaidi ya aina kubwa yenye matunguu makubwa.

««« Makala iliyopita: Ufanye nini na majani yaliyofyekwa? Makala inayofuata: Welwitschia mirabilis – ukulima wa kisukuku »»»

Ijumaa 22.7.2011 08:56 | chapa | Maelekezo juu ya uoto wa mimea

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.