Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Welwitschia mirabilis – ukulima wa kisukuku

foto

Welwitschia

Welwitschia (Welwitschia mirabilis) ni mmea wa kale unaolimwa katika eneo dogo la ukanda wa mkoa wa pwani wa Bahari ya Atlantic nchini Namibia na Kusini mwa Angola. Welwitschia kiukweli ni mti, ingawa hauonekani kama mti kwa mtazamo wa haraka wa kwanza. Mmea wote una shina moja fupi ambalo hutoa majani mawili – haya yanaonekana kama riboni mbili kubwa zenye mawimbi yaliyochakaa, ncha kumba. Welwitschia wakati mwingine unaonekana kama rundo takataka!

foto

Welwitschia

Mmea wakati wote uko katika kipindi cha kuota (hata wakati wa kipindi cha kuzaa) – ambao kwa kiasi kikubwa ni kawaida mingoni mwa mimea. Welwitschia ni aina ya dioecious na hivyo mimea miwili (mmea wa kike na wakiume) ni muhimu kwa kutengeneza mbegu. Maua yako kwenye pia (kama yake ya mti wa msonobari au cycads) ambayo iko kwenye axil ya majani.

Pia za kike hupasuka zinapokomaa na kutoa mbegu nyepesi zenye mbawa, ambazo husambazwa kwa urahisi na upepo.

Iko kwenye sehemu ya mimea ya asili – Gnetophyta, ambayo inahusiana kabisa na conifers (Pinophyta). Gnetophyta ina genuses 3 tofauti inapokuja kwenye mwonekano: Gnetum – lianas with large simple leaves, Ephedra – shrubs and the Welwitschia itself.

Welwitschia linatokana na jina Slovene botanist Friedrich Welwitsch ambaye aliigundua mwaka 1860. Welwitschia iko kwenye koti ya majeshi ya Namibia.

foto

Mbegu za Welwitschia

Welwitschia inachukuliana kabisa na hali za jangwani. Haitegemei mvua na hupata maji ya kutosha kutoka kwenye mvuke unaotoka kwenye bahari. Ukweli huu unatakiwa kuuweka akilini unapootesha Welwitschia. Sababu ya pekee inayofanya ulimaji wa Welwitschia ushindwe ni wakati unapopewa maji mengi kupelekea kuoza kwa mmea. Hivyo basi ni muhimu kwamba mbegu zinapandwa kwenye tabaka la mshanga (mbegu ziwe kati ya mm 2–5 katika kipenyo) kwasababu kuweka maji mengi ni kikwazo kikubwa cha ukuaji. Ni muhimu kumwagilia Welwitschia kwa uangalifu mkubwa – na ni bora hata kuloanisha kwa ulaini. Mbegu huota ndani ya wiki moja. Mimea inaweza pia kuoteshwa kwenye vizingiti vya madirisha ikiangalia kusini. Unapootesha Welwitschia, unatakiwa kuwa mvumilivu sana kwani mmea huu hukua taratibu sana – hakika ni dinasau kwa kuzungumza. Kama itapewa Mwanga wa kutosha na siyo maji wengi, mmea hakika unaishi muda mrefu zaidi yako!

««« Makala iliyopita: Upandaji wa matunguu na miche ya maua

Jumanne 26.7.2011 10:32 | chapa | Mimea ya kigeni

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.