Michikichi Parajubaea torallyi
Parajubaea torallyi ni mchikichi mgumu wa kuvutia kutoka Marekani ya Kusini. Hata hivyo, hulimwa kwa kiwango kidogo nje ya eneo lake la asili, Bolivia, kutokana na ukubwa wa mbegu zake ambazo usafirishaji wake unatumia gharama kubwa.
Asili yake ni Bolivia, hukua kwenye ukame na vumbi, kati ya bonde la Andean kwenye mwinuko wa m 2700–3400 kutoka kwenye usawa wa bahari. Spishi hii ya mchikichi ni ndefu ambayo haijawahi kutokea sehemu yoyote duniani. Mara chache kiwango cha joto hupanda zaidi ya nyuzijoto 20. Kiwango cha joto mara kwa mara hushuka hadi nyuzijto –7 kwenye miezi ya baridi (Julai na Agosti) na mvua kwa mwaka ni mm 550 tu.
Ustahimilivu wake wa ukame, joto, baridi, barafu, na hali nyingine mbaya, na uwezo wake wa kuhifadhi mwonekano wake, husababisha baadhi ya watu kusema kuwa mchikichi huu maarufu siyo tu una uwezo mkubwa kama mmea wa mapambo, lakini pia , unaweza kuwa moja ya mandhari ya michikichi inayovutia kwa maeneo yenye hali ya hewa ya joto sana na pia yenye joto kiasi. Kwenye maeneo ambayo barafu hutokea inahitaji kukingwa na baridi au kuhifadhiwa kwenye mazingira ambayo hayana baridi. Imearifiwa kwamba Ulaya kiwango cha baridi hufikia nyuzijoto –3. Kiwango cha chini cha joto ambacho mchikichi huu uliweza kupona shambani kilikuwa nyuzijoto –8. Mimea hii ilipoteza majani yake yote lakini ilipona na kwenye kipindi cha uotaji, majani mapya yalitokea!
Huko Bolivia mchikichi huu hukua hadi kufikia urefu wa m 14, na shina lenye upana wa sm 25–35. Michikichi ambayo umri wake ni miaka 100 na zaidi, hukua na kufikia urefu wa m 30 na shina lenye upana wa sm 50. Sehemu ya juu nzuri ina takribani majani 20 na baadhi yake huenda juu hadi mita 5! Hata hivyo mimea aina hii inayokuzwa nje ya Bolivia ni midogo.
Kuna jamii mbili tofauti katika mazingira ya asili ambayo hutofautiana zaidi kwenye saizi ya matunda na hivi karibuni zimeelezewa kama aina mbili tofauti, yenye matunda madogo P. torallyi var. microcarpa na yenye matunda makubwa P. torallyi var. torallyi. Aidha tofauti ya mwonekano wake siyo muhimu, var. microcarpa haifikii saizi ya mchikichi wa matunda makubwa, lakini kwa upande wa uimara wake haishindwi chochote. Mbegu inatabia ya kutotegemea vitu vingine katika ukuaji. Ingawa kukua kwake kunaweza kuwa siyo kwa kawaida, mbegu inaweza kuchipua kwa urahisi inapokuwa imepandwa kwenye hali ya hewa sahihi, i.e. nje ya makuo, imefukiwa nusu, na unyevunyevu kiasi. Na uangalizi mzuri, kwenye ubaridi hasa katika maeneo yenye hali ya hewa ya joto kiasi na jua, miche itarefuka kwa haraka, mashina manene, majani magumu. Ustahimilivu wake wa ukame, joto, baridi, barafu, na hali nyingine mbaya, na uwezo wake wa kuhifadhi ukijani wake, husababisha baadhi ya watu kusema kuwa mchikichi huu maarufu siyo tu una uwezo mkubwa kama mmea wa mapambo, lakini pia , unaweza kuwa moja ya mandhari ya michikichi inayovutia kwa maeneo yenye hali ya hewa ya joto sana na pia yenye joto kiasi.
Parajubaea torallyi ni mmea maarufu sana wa mapambo na mara nyingi hupandwa kwenye hifadhi na njia za kutembea kwa miguu. Ecuador na Kusini mwa Colombia, Parajubaea cocoides mara nyingi hupandwa kwenye mwinuko wa mita 2500 hadi 3000 – huu ni mchikichi unaokua kwa taratibu na huvumilia baridi kiasi. Kama ilivyo sawa na Parajubaea torallyi na kama ambavyo uasili wake haujulikani, imekubalika kwamba ni Parajubaea torallyi.
Saizi ndogo ya spishi hii ya mchikichi ni Parajubaea sunkha ambayo iligundulika mwaka 1996. hurefuka kwa urefu wa mita 8 tu na hutokea kwenye bonde la Andean katika mkoa wa Vallegrande, wilaya ya Santa Cruz, Bolivia, ambako mwinuko ni wake m 1700–2200. imekuwa wakati wote ikijulikana kimakosa kama Parajubaea torallyi hadi hivi karibuni utafiti ulipofanyika na kupewa jina la Parajubaea sunkha.
Mchikichi wa jenasi Parajubaea hulimwa kwa urahisi. Njia nzuri ya ukuzaji wake ni kwa kutumia mbegu. Hata hivyo unatakiwa kuwa mvumilivu kutokana na mbegu yake kuchipua kwa taratibu, na huchukua takribani mwaka hadi mwaka na nusu kufanya hivyo. Baadhi ya mbegu huanza kuota ndani ya mwezi, lakini nyingine huchukua mwaka au hata miaka miwili kuanza kuchipua. Ikiwa ni spishi ya mchikichi ya hali ya joto, ni bora ihifadhiwe kwenye kiwango cha chini cha joto, kwa kuwa kiwango cha juu cha joto (kama ilivyo kwa spishi nyingine za michikichi) inaweza kuwa na madhara katika hatua za ukuaji. Kiwango cha juu cha joto kinaashiria msimu wa ukame, ambao siyo mzuri kwa ukuaji.
Kabla ya kupanda, mbegu ni lazima ziwekwe kwenye maji yenye joto la takribani nyuzijoto 20 kwa kati ya siku 5 hadi 7. kwa aina ya mbegu kuwa ni lazima iwekwe kwenye maji kwa karibu wiki mbili. Maji lazima yabadilishwe kila siku. Mbegu zinaweza pia kukatwa kidogo kuruhusu ukuaji bora.
Kuloanisha mbegu kwenye maji kutahitimisha kipindi cha kudumaa kwa mbegu na will inaugurate the rainy season, ambao ni msimu mzuri kwa ukuaji. Kudumaa kunazuia mbegu kuanza kuota wakati wa msimu wa kiangazi Bolivia (msimu wa baridi Juni hadi Oktoba)
Baada ya kulowanisha mbegu ni lazima ipandwe kwenye chungu au mfuko wa plastiki – hakikisha kuwa nusu ya mbegu imefunikwa na udongo na ziweke kwenye joto la nyuzijoto 10 hadi 20.
Hali inayovutia kwa ukuaji mzuri ni utofauti kiwango cha joto kati ya mchana (juu) na usiku (chini). Mara tu baada ya mbegu kupandwa, zisimwagiliwe maji mengi, maana maji mengu yanaweza kuharibu michikichi michanga. Tofauti iliyopo kati ya kilimo cha Parajubaea na spishi zingine za michikichi ni kwamba kiwango cha joto kinachohitajika ni cha chini na pia maji ni kwa kiasi kidogo.
Baada ya kupanda, mbegu ni lazima ziangaliwe kila baada ya wiki tatu hadi nne na mbegu zilizochipua ziwekwe kwenye vyungu vya peke yake. Baadhi ya wakulima wa michikichi wametoa ushauri ufuatao kuhusiana na mbegu ambazo hazichipui ndani ya miezi sita:
Acha kuweka maji na ruhusu udongo ukauke kwa miezi kadhaa. Zitoe mbegu kwenye udongo, zirudishe tena kwenye maji zikae humo kwa wiki moja kisha zipande tena. Mbegu hizi lazima zianze kuchipua ndani ya nusu mwaka ujao. Kama baadhi ya mbegu bado hazichipui, rudia tena na mbegu zingine zilizobaki zitachipua baada ya msimu ujao wa mvua.
Kiwango cha ukuaji wa mbegu za Parajubaea ni karibu 100%, unachotakiwa ni kuwa na uvumilivu wa kutosha, na ruhusu msimu wa ukame kwa zile mbegu goigoi!
Mara unapokuwa na michikichi michanga, ni vigumu laikini kumbuka kwamba usiumwagilie maji sana. Michikichi michanga hupendelea mazingira ya kawaida (kwenye mahali pake pa asili hukua chini ya kivuli cha michikichi mikubwa, hata hivyo mimea iliyokua kuhitaji jua.
Jenasi Parajubaea ni moja kari ya michikichi ambayo iko hatarini Kusini mwa Marekani. Sababu kuu hasa ni uharibifu maliasili, kuongezeka kwa mahitaji ya ardhi kwaajili ya kilimo, viwanda vya mbao na ulishaji mifugo. Hii michikichi hutokea kwenye eneo dogo sana, inayofanya kuangaliwa kwa makini zaidi dhidi ya hatari ya kutoweka. Kutokana na ukubwa wa mbegu za mimea hii pia uenezaji wake ni mdogo. Mnyama muhimu sana anayesaidia michikichi hii kuenea kwenye maeneo mapya ni Spectacled Bear (Tremarctos ornatus), hata hivyo wanayama hawa pia wanaogopeshwa na shughuli za binadamu.
««« Makala iliyopita: Khasi Pine (Pinus kesiya) Makala inayofuata: Michikichi inayostahimili baridi Rhapidophyllum hystrix »»»
Jumapili 9.8.2009 11:36 | chapa | Michikichi
Kuhusu KPR
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.