Michikichi inayostahimili baridi Rhapidophyllum hystrix
Rhapidophyllum hystrix ni spishi kuu ya mchikichi inayostahimili baridi kali. Kuna spishi moja tu kwenye jenasi Rhapidophyllum. Maskani ya asili ya mchikichi huu ni maeneo yenye unyevunyevu ya sehemu za Kusini- Mashariki mwa Marekani. Hata hivyo, shukrani kwa tabia yake ya kuvumilia baridi kali ambayo iko chini kama nyuzi joto – 20, ni mmea wa bustani unaojulikana sana duniani, hasa hasa Ulaya.
Ni spishi ngumu za mchikichi, ambayo inarefuka kwa mita 1–3 tu ikiwa na matawi matawi mengi kwenye shina. Rhapidophyllum hystrix ni kichaka kidogo cha mchikichi cha kufurahisha, kinachozalisha vichipukizi. Hayo mashina mengi yanatengeneza kichaka chenye muundo wa duara ambacgo hakiko wazi na hakipitiki.
Mchikichi mwembamba hautengenezi shina lakini badala yake huwa na sehemu ya juu ambayo hukua kwa taratibu hadi kufikia urefu wa m 1.2 kwenda juu na upana wa karibu sm 17.8. Mashina hutengenezwa na majani ya zamani, nyuzinyuzi, na miba mirefu myembamba.
Kwa kawaida iko wima lakini kwa vichaka vya zamani vinaweza kukua chini kwa chini usawa wa ardhi wakati matawi yanaposhindana kupata mwanga na nafasi. Kwa jinsi shina linavyozidi kuwa kubwa ndivyo pia miba myembamba inavyozidi kukua katikati ya majani.
Mbegu lazima zioteshwe kwenye udongo wenye unyevunyevu na kuhifadhiwa kwenye joto karibu ya nyuzijoto 20. Katika miaka 3 ya mwanzo, inashauriwa kuwa michikichi michanga ihifadhiwe mbali na barafu. Mchikichi mwembamba hupendelea sehemu zenye jua au kivuli, lakini kwa ujumla huhitaji jua zaidi kadri latitudo inavyoongezeka. Hata hivyo huonekana vizuri ikiwa kwenye kivuli kiasi.
Ikioteshwa kwenye eneo lenye jua wakati wote sehemu yake ya juu ina tabia ya kubanana na majani yake kupoteza rangi yake ya kijani kibichi. Mimea yenye umri wa zaidi ya miaka 3 inaweza kuwekwa nje kwenye bustani kwa kipindi cha mwaka mzima kama unaishi kwenye eneo ambalo kiwango chake cha joto hakishuki chini ya nyuzijoto hasi 10.
Kwenye maeneo ya baridi, unahitajika kuwekewa vizuizi vya kutosha vya kuzuia baridi endapo kiwango cha joto kitashuka chini ya nyuzi joto –10. Ukiwa kama mchikichi unaostahimili barafu, unahitaji udongo uliokauka vizuri na ni lazima uwe upande kusini. Adui mkubwa wa mchikichi huu wakati wa baridi siyo barafu bali ni udongo wenye maji mengi. Mchanagnyiko wa kiwango cha chini cha joto na maji mengi huathiri mizizi. Mchikichi huu unaweza kuishi kwenye baridi nyuzi joto –15 hadi –20. kiwango cha chini cha joto kilichowahi kurikodiwa, ambacho michikichi hii iliweza kuishi ilikuwa nyuzi joto –28.
michikichi inayostahimili baridi
inauzwa
««« Makala iliyopita: Michikichi Parajubaea torallyi Makala inayofuata: Indian Lotus (Nelumbo nucifera) »»»
Jumapili 9.8.2009 11:39 | chapa | Michikichi
Kuhusu KPR
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.