Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Indian Lotus (Nelumbo nucifera)

foto

ua ya Indian Lotus

Indian Lotus (Nelumbo nucifera) ni mmea unaovutia wa majini wenye majani ya rangi ya kijani yanayoelea juu ya maji. Maua ya rangi ya waridi kwa kawaida yanapatikana kwenye mashina myembamba yanayokua kwa sentimeta kadhaa juu ya maji.

Maua ya Indian Lotus hutumika na wafuasi wa madhehebu ya Budha wakati wa sherehe za kidini. Mmea wote hufaa kwa matumizi ya binadamu, ingawa hasa mbegu na mzizi hutumika kwenye mapishi ya kitamaduni Kusini-Mashariki yote ya Asia. Indian Lotus ni mmea wa paludal ambapo unaweza kuoteshwa kama vile unavyooteshwa lily ya majini yanayonukia. Siyo vigumu kuotesha mmea huu kwenye hali zetu; mtu ni lazima ajue ni kwa namna gani!

Kuotesha Indian Lotus kwa kutumia mbegu, ni lazima gamba gumu la nje likwaruzwe kidogo (kufuta au kusugua) kwa msasa. Hii inaruhusu maji kupita kwa urahisi ambapo bila ya hayo mbegu yaiwezi kuota. Kama gamba gumu litaendelea kuwepo mbegu hiyo itakuwepo karne kwa karne. Hata hivyo mbegu hiyo ikiwekwa kwenye maji itachukua miaka kadha kuchipuka.

foto

Kuotesha mbegu za Indian Lotus

Utajuaje kama umekwaruza mbegu za kutosha? Mtu anaweza kutambua kwa kuangalia saizi ya ukuaji wa mbegu mara tu zinapowekwa kwenye maji. Kama mbegu inaongezeka saizi mara mbili ndani ya saa 24, hakuna haja ya kukwaruza mbegu zingine. Kama hazikuongezeka, basi unahitajika kukwaruza mbegu nyingine zaidi, weka tena mbegu kwenye maji kwa saa 24 zingine, na kasha angalia saizi yake. Hatua hii ni lazima irudiwerudiwe hadi mbegu zinongezekesaizi yake mara mbili.

Mbegu zinahitaji maji tu…

Mara tu hatua ya kukwaruza inapokamilika, loweka mbegu kwenye chombo chenye maji. Kiwango kizuri cha joto cha maji katika hatua za awali za kuchipuani kati ya Nyuzijoto 27 na 28 (hata kama mbegu inaweza kuongeza saizi yake mara mbili kwenye kiwango cha nyuzijoto 20 tu). Katika kiwango hiki cha joto mbegu hukua haraka na ndani ya iki vichipukizi vitaonekana. Angalia foto kwenye
.

Punde jani la kwanza litakapochomoza, panda mbegu hiyo iliyochipua aidha kwenye udongo au kwenye chombo chenye changarawe (chombo cha kuhifadhia samaki, dimbwi). Kiwango cha maji kwenye chombo ni lazima kiwe angalau sm 30 kutoka udongo ulipoishia. Kama chombo kinachotumika ni kile cha kutunzia samaki, Indian Lotus inaweza kukua kwa urahisi kwenye chombo hicho pamoja na samaki.

Polepole, kadri mmea unavyokua, ndivyo utavyohitaji nafasi zaidi. Unaweza kukuza kwenye bwawa bustanini, kwenye nyumba ya kuhifadhia mimea, au kwenye eneo lolote lile mbali na baridi. Kiwango kizuri cha joto cha kukuzia Indian Lotus ni kati ya nyuzijoto 20 na 35.

Indian Lotus inaweza kukuzwa kwenye bustani katika kipindi chote cha mwaka kwenye maeneo mengi Afrika. Kiwango cha chini cha joto kisishuke chini ya nyuzijoto 0.

Njia bora ya kuotesha Indian Lotus ni kwa kutumia mabeseni yaliyozibwa vizuri linalobeba maji kuanzia lita 60 au 80. Tumia njia ifuatayo: Weka mbegu iliyochipua kwenye udongo au chombo cha kuhifadhia samaki ndani ya chungu cha maua na kisha weka chungu cha maua ndani ya beseni . kwa matokeo mazuri ya ukuaji, beseni lijaze maji hadi juu.

Faida ya kutumia beseni lilozibwa vizuri ni kwamba linaweza kuwekwa sehemu yoyote kwa urahisi. Mmea wa Indian lotus unaweza kukua kwa urahisi mahali popote – hata kwenye nyumba.

««« Makala iliyopita: Michikichi inayostahimili baridi Rhapidophyllum hystrix Makala inayofuata: Maembe ya Indonesia »»»

Jumapili 9.8.2009 11:54 | chapa | Mimea inayotumia maji mengi na mimea ya majini

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.