Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Maembe ya Indonesia

Katika Kisiwa cha Borneo huko Indonesia kuna spishi za mwembe zipatazo 34 (Mangifera) ambazo hutokea kiasili kwenye kisiwa. Idadi kubwa ya spishi hizi ziko hatarini kupotea kutokana na uharibifu wa misitu. Baadhi ya spishi kama vile Kalimantan Mango (Mangifera casturi) tayari imepotea porini.

Baadhi ya miembe mingine kutoka Borneo mfano Mangifera griffithi (inajulikana kwa majina la kienyeji: asem raba, na romian), Mangifera pajang (asem payang), Mangifera quadrifida (asem kipang) na Mangifera torquenda (asem putaran).

Fragrant Mango (Mangifera odorata) ni spishi ya mwembe inayojulikana sana mara kwa mara inakua Kusini –Mashariki mwa Asia. Ni mchanganyiko wa mwembe unaolimwa sana (Mangifera indica) na Horse Mango (Mangifera foetida). Inajulikana kwa majina ya kienyeji : kuweni, kuwini (katika lugha ya Kiindonesia); kweni, asam membacang, macang, lekup (katika lugha ya Malay); kuwini, ambacang, embacang, lakuik (katika lugha ya Minangkabau); kuweni, kebembem (katika lugha ya Betawi); kaweni, kawini, bembem (katika lugha ya Kisudani); kaweni, kuweni, kweni (katika lugha ya Javan); kabeni, beni, bine, pao kabine (katika lugha ya Maduri ), kweni, weni (katika lugha ya Kibalini); mangga kuini (Kaskazini Sulawesi); na kuini, guin, koini, kowini, koine, guawe stinki, sitingki, hitingki (katika visiwa vya Maluku).

««« Makala iliyopita: Indian Lotus (Nelumbo nucifera) Makala inayofuata: Kukuza mwembe kutoka mbegu »»»

Jumatatu 31.8.2009 17:30 | chapa | Mimea ya kigeni

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.