Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Kukuza mwembe kutoka mbegu

Unatakiwa kupanda mbegu iliyovunwa vizuri, ili kupata matokeo mazuri ya uotaji. Loanisha mbegu kwenye maji yenye kiwango cha joto karibu nyuzijoto 20–25 kwa muda wa takribani saa 2–6.

Baada ya kuziloanisha zipande mbegu hizo kwenye udongo (udongo mwepesi, kichanga) na hakikisha kiwango cha joto katika chungu kiko angalau nyuzijoto 20–25. Mbegu zinaanza kuchipua ndani ya wiki 1–3. Miche michanga lazima ihifadhiwe kwenye eneo lenge kiwango cha kati cha jua.

Kama unaishi kwenye sehemu yenye joto, unaweza kuotesha mwembe kwenye bustani yako. Kama unaishi kwenye maeneo ambayo yana baridi au mara nyingine barafu hutokea, ni muhimu kuweka miche ya mwembe ndani au katika nyumba ya kuhifadhia mimea.

««« Makala iliyopita: Maembe ya Indonesia Makala inayofuata: Embe Kalimantan, Kasturi (Mangifera casturi) »»»

Jumanne 1.9.2009 07:01 | chapa | Mimea ya kigeni

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.