Embe Kalimantan, Kasturi (Mangifera casturi)
Embe Kalimantan (Mangifera casturi) au kienyeji unajulikana kama Kasturi ni tunda la mti wa matunda ya msimu wa joto, wenye urefu wa takribani mita 10–30, unapatikana kwenye eneo dogo la Banjarmasin, Kusini mwa Borneo (Indonesia). Siku hizi miti hii imeadimika sehemu za porini kutokana na kukatwa katwa kinyume cha sheria. Hata hivyo bado inalimwa kwa kiasi kidogo katika eneo hili kutokana na utamu wa matunda yake.
Saizi ya matunda ya embe Kalimantan (Mangifera casturi) ni ndogo ikilinganishwa na spishi zingine za maembe. Uzito wake kwa kila tunda ni kati ya gramu 50 hadi 84. Likiwa bado bichi, rangi ya tunda ni kijani – linapoiva rangi yake hubadilika na kuwa kahawia au zambarau iliyokolea na lina ndozi inayong’aa. Muundo wa rangi pia ni moja ya utambulisho wa aina za M. casturi. Kuna aina 3 za Mangifera casturi – Kasturi, Mangga Cuban na Pelipisan. Unaojulikana sana ni Kasturi kwa sababu ya harufu yake. Mangga Cuban na Pelipisan mara nyingi huonekana kama spishi mbili tofauti. Pelipisan unaweza hatahivyo kutambulika kwa harufu tamu kama Kasturi ambayo inaashiria kuwa tunda hilo ni kama mchanganyiko wa Kasturi. Tafiti zaidi zinahitajika kufanyika kutafsiri na kuweka gredi.
Ubichi wa tunda hili uko kwenye rangi ya chungwa na mfumo wa harufu tamu ya kipekee. Kama tukilinganisha Kasturi na Embe (Mangifera indica), Kasturi lina radha tamu kiasi likini ina radha imara na harufu laini. Tunda la Kasturi bichi lina nyuzi nyuzi nyingi.
Kasturi unafahamika sana kwa baadhi ya watu wa Borneo Kusini na vile vile katika mkoa wa jirani. Harufu ya matunda ni nzuri, kuna wimbo wa zamani unaotokana na matunda haya: “Seharum kasturi, seindah pelangi, semuanya bermula.” Ikiwa na maana: “Oh, harufu kama Kasturi, uzuri kama upinde wa mvua. Penzi hili limeanza safari yake.”
Shughuli za ukataji kinyume cha sheria umesababisha mtu huu kuadimika porini. Miti ya embe Kalimantan iko kwenye hatari ya kupotea kwa kukatwa kutokana na wingi wa mbao zake. Miti mara nyingi hulimwa kwa kiwango kidogo na watu wa kawaida kwenye bustani zao uani au mashamba madogo.
Siyo kama ilivyo kwa upandaji wa miti mingine ya matunda ya msimu wa joto, Embe Kalimantan halipandwi kwenye mashamba makubwa Indonesia kutokana na ukuaji wake kuwa wa taratibu. Mashamba makubwa ya Embe Kalimantan yanapatikana eneo la Mataraman tu, wilaya ya Banjar (wilaya ya Banjar siyo sawa na wilaya ya Banjarmasin). Watu wa Mataraman walijaribu kupanda kuwango kidogo 1980 na mavuno ya kwanza yalikuwa mwaka 2005. Ingawa tunda hili kiasili linapatikana kwa wingi bado halitoshelezi mahitaji.
Matumizi ya miti ya miembe ya Kalimantan ni kwa matunda na kuni. Ingawa miti iliyozeeka inaweza kuwa na shina linaloongezeka kwa mita, watu wa Banjar (kundi la kabila la ndani na pwani ambalo liko Kusini mwa Borneo), hupenda kutumia matunda tu kutokana na mti wake kuchukua muda mrefu kukua. Kutokana na sababu hiyo, watu wa Banjar huchagua miti mingine kama chanzo chao cha nishati ya kuni yenye ubora sawa au ubora zaidi wa mbao. Kulifikia tunda sirahisi sana kutokana na mti wa Kasturi kuwa mrefu sana na hivyo mtu anatakiwa kukwea juu sana kulifikia – tunda linalodondoka chini lenyewe linakuwa halina ubora.
Matunda yanaweza kuliwa yakiwa mabichi au yakatengenezwa kama jem ya Kasturi. Hata hivyo uuzaji wake ni wa nadra sana kwenye masoko, kutokana na wakulima kula wao wenyewe. Bidhaa zingine zinazotokana na maembe ni puree, jem, juice au dodol (mapishi ya kiasili). Bidhaa hizi hata hivyo ni ngumu kuzipata kutokana na mahitaji ya matunda bichi wakati wote kuwa makubwa na ni moja ya matunda yanayopendwa sana na watu wa Banjar. Matunda hayo pia ni ya ghali kidogo, lakini kwa watu wa Banjar ni sawa kwa pesa zao kwasababu ya radha yake ya ajabu!
««« Makala iliyopita: Kukuza mwembe kutoka mbegu Makala inayofuata: Chai ya China – Lima chai yako mwenyewe! »»»
Jumatatu 7.9.2009 12:48 | chapa | Mimea ya kigeni
Kuhusu KPR
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.